Mwakilishi Marekani kutoka jimbo la Texas Sheila Jackson Lee afariki dunia

Mwakilishi wa Marekani Sheila Jackson Lee Mdemokrat wa Texas wakati wa uhai wake katika chakula cha jioni cha Chama cha Waandishi wa White House Washington Hilton huko Washington, DC, Aprili 29, 2023.

Mwakilishi wa muda mrefu wa Marekani kutoka jimbo la Texas Sheila Jackson Lee  ambaye alisaidia kuongoza juhudi za kutambua Juni kumi na tisa  kama sikukuu ya kitaifa, amefariki dunia.

Mwakilishi wa muda mrefu wa Marekani kutoka jimbo la Texas Sheila Jackson Lee ambaye alisaidia kuongoza juhudi za serikali kuu kuwalinda wanawake dhidi ya unyanyasaji wa majumbani na kutambua Juni kumi na tisa kama sikukuu ya kitaifa, amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 74.

Lillie Conley, mkuu wake wa utumishi, alithibitisha kuwa Jackson Lee, ambaye alikuwa na saratani ya kongosho, alifariki huko Houston Ijumaa usiku na familia yake ikiwa karibu naye.

Mdemokrat huyo alikuwa amewakilisha jimbo lake la uchaguzi lenye makao yake mjini Houston na jiji la nne kwa ukubwa nchini Marekani tangu mwaka 1995. Hapo awali alikuwa na saratani ya matiti na alitangaza pia kupatikana na saratani ya kongosho Juni 2.