Mvua kubwa sana imenyesha katika msimu huu nchini Chad baada ya kipindi cha miaka 30 imeacha sehemu za mji mkuu N'Djamena kupitika kwa kutumia boti pekee na kuwalazimu maelfu kukimbia makazi yao yaliyofurika maji katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, kulingana na mashirika ya misaada na shirika la taifa la hali ya hewa wa serikali.
Katika wilaya ya nane ya N'Djamena, familia zimerundikana kwenye boti za mbao kuvuka mitaa ambayo imejaa maji ya mafuriko tangu mwisho wa Julai.
Mafuriko si jambo lisilo la kawaida wakati wa msimu wa mvua katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati, ambayo kwa kawaida huanza Mei hadi Oktoba katika maeneo yake ya kati na kusini. Lakini wakati huu, mvua ilikuja mapema na ilikuwa nyingi sana na kwa haraka ikajaza mifereji ya maji na madimbwi.