Mawaziri hao vile vile watajadiliana kuhusu uwezekano wa Syria kurudi kwenye muungano wa nchi za kiarabu, zaidi ya mwongo mmoja tangu kufutiwa uanachama.
Mkutano huo utafanyika Jumapili.
Unajiri wakati baadhi ya nchi za kiarabu zikiwemo Misri na Saudi Arabia, zikiwa zimeanzisha ushirikiano mpya wa kidiplomasia na rais wa Syria Bshar Al-Assad.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu waliitembelea Damascus wiki chache zilizopita kwa mazungumzo yanayohusu Syria kurudi kwenye muungano huo wenye nchi wanachama 22.
Syria iliondolewa kwenye muungano huo miaka 12 iliyopita na kuwekewa vikwazo kutokana na machafuko yaliyopelekea vifo vya karibu watu nusu milioni na wengi kukoseshwa makazi.