Muslim Brotherhood ya Misri inaripoti kukamatwa wafuasi wake

Polisi wa Misri wa kupambana na ghasia wakikabiliana na waandamanaji.

Kundi la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku Misri lakini linawagombea uchaguzi huru, linadai kwamba vikosi vya usalama vimewakamata mamia ya wanaharakati wake kote nchini, kuanzia Ijuma hadi Jumamosi, baada ya kutokana na ghasia wakati wa mikutano kadhaa ya kampeni.

Vyombo vya habari vinripoti kutokea ghasia katika miji tofauti karibu na Cairo na Alexandria na kiasi ya watu 10 wamejeruhiwa katika mapambano kati ya wandamanaji na vikosi vya usalama.

Ukurasa wa mtandao wa Muslim Brotherhood, wa IkhwanOnlie unadai wanachama wake 250 wamekamatwa na shirika la habari la Associated Press linaripoti kwamba kuna hali ya mvutano mkubwa wakati siku ya uchaguzi wa bunge inakaribia hapo Novemba 28.

Ukurasa huo unaripoti pia, vikosi vya polisi vimepiga marufuku mikutano ya hadhara au mandamano yatakayounga mkono Muslim Brotherhood. Ripoti za polisi zinaeleza kukamatwa kwa mamia ya watu katika miji mbali mbali lakini haizkutaja majeruhi wala kupiga marufuku maandamano.

Muslim Brotherhood ina viti 88 katika bunge la sasa la Misri, na uchaguzi huu unachukuliwa ni mtihani na matayarisho ya uhaguzi wa rais hapo mwakani ambapo Rais Hosni Mubarak anatarajiwa kugombania tena kiti chake.

Marekani imeihimiza serikali ya Misri siku ya Jumatatu kuruhusu mikusanyiko ya amani ya kisiasa na kuruhusu vyombo vya habari kuripoti kwa uwazi na uhuru.