Museveni atishia kuondowa majeshi Somalia

  • Leylah Ndinda

Balozi Augustine Mahiga, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametishia kuondowa majeshi yake kutoka Somalia ikiwa tarehe ya uchaguzi haitobadilishwa ili kuruhusu matayrisho kufanyika vizuri

Kiongozi huyo wa Uganda akihutubia mkutano wa wajumbe kutoka jopo la wajumbe wa matifa yanayoshughulikia suala la Somalia, alisema ikiwa uchaguzi wa bunge na rais utafanyika kama ulivyopangwa na Umoja wa Matiafa kabla ya mwisho wa mwaka huu basi wanaharakati wa Al Shabab watatumia muda huo kushamnbulia na kuvuruga utaratibu wote.

Hata hivyo mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somali, Balozi Augustine Mahiga amesisitiza haja ya kufanyika kwa uchaguzi kwa haraka na kuishutumu serikali ya mpito kwa kutoweza kutekeleza ahadi na majukumu yake yaliyopangwa miaka miwili iliyopita.

Akizungumza na sauti ya amerika huko Kampala Bw Mahiga alisema ni lazima kuendelea kuwahimiza viongozi wa Somalia kusikilizana na kuendelea na utaratibu wa kudumisha amani na uthabiti nchini mwao.