Museveni amekutana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud katika ikulu ya rais ya Entebbe.
Museveni amesema kwamba Uganda itaisaidia Somalia kwa kila hali kuhakikisha kwamba changamoto za kiusalama nchini Somalia zinatatuliwa.
“Tutaendelea kuwapa silaha ili kukabiliana na ukosefu wa usalama. Viongozi katika eneo hili tutaendelea kuwapa silaha. Mnastahili kuwa na mpang wa namna ya kujenga jeshi lenu. Watu wanastahili kujenga jeshi lao ili kujilinda.
Somalia kushinda Al-shabaab katika mda wa miezi 6
Rais wa Somalia Mahamud amesisitiza kwamba anaushukuru Umoja wa Afrika kwa kutuma wanajeshi nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al-shabaab.
“Tunashukuru jeshi la Uganda UPDF kwa kutekeleza jukumu kubwa sana la kuimarisha usalama nchini Somalia. Jeshi la Somalia limepiga hatua kubwa katika kujiimarisha na raia wanashirikiana vyema na jeshi.” Amesema rais Mahamud.
Rais wa Somalia ameeleza matumaini kwamba jeshi la nchi hiyo litawashinda wapiganaji wa Al-shabaab katika muda wa miezi sita ijayo.
Vita dhidi ya Ebola Uganda
Museveni vile vile amesema kwamba Uganda imepiga hatua nzuri katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Ebola.
“Ni rahisi kukabiliana na virusi vya Ebola kuliko Covid-19 kwa sababu ebola vinasambaa pale watu wanapogusana na wala sio kupitia hewani.” Amesema Museveni.