Muhula wa kwanza wa Obama

Rais Barack Obama, wa Marekani alipomshinda mgombea kiti wa chama cha Republican Mitt Romney, ili kuingia madarakani kwa mhula wa pili akiwa na familia yake.

Rais Barack Obama anaapishwa Januari 21 kwa muhula wa pili akiwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuchaguliwa kwa mara ya pili na hivyo kuifanya sherehe hiyo kuwa ya kihistoria

Sherehe hizo ni za kihistopia pia kwa vile zinafanyika siku ya kuzaliwa kwa Martin Luther King, mtetezi mkuu wa haki za kiraia hapa Marekani
.
Hata hivyo matatizo yaliyokumba nchi hii kwa miaka minne iliyopita imemsababisha kuzeeka kwa ghafla na kujaa mvi kichwani na kutupelekea kutafakari ni matatizo gani yaliyompelekea kuwa katika hali hiyo.

Wataalamu na wachambuzi wanasema miaka minne ya utawala inawafanya marais wa Marekani kuzeeka mara mbili au mara tatu haraka zaidi ya watu wa kawaida.
Alipochukua madaraka mwaka 2009 Rais Obama alikabiliana kwanza na tatizo la mzozo mkubwa wa kiuchumi, Professa Richard Mshomba wa chuo cha la sale anasema

Your browser doesn’t support HTML5

Mhula wa kwanza wa Obama


“Changamoto kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba alirithi uchumi ambao ulikuwa unaporomoka kwa kasi kubwa sana. Na alichofanikiwa kufanya ni kupitisha ni kupitisha kichocheo cha uchumi cha dola karibi milioni 800.”

Hisa ziliporomoka, mabeki makubwa kukabiliwa na matatizo na viwanda vya magari vilihitaji msaada.

“ Vilihitaji kupatiwa oxijeni na kuongezewa damu. Huduma hizo zilikuja kwa njia ya serikali kuwekeza dola bilioni 62, kwa kununuwa hisa za kampuni hizo.”

Kuongezea matatizo hayo, soko la nyumba liliporomoka watu wakashindwa kulipa madeni yao na kupoteza nyumba zao. Profesa Mshomba anasema Rais Obama aliwaokowa wamiliki nyumba kwa njia nyingi hasa kwa kupitisha sheria zinazowabana watowa mikopo, na msaada kwa walopoteza makazi yao.

Kuapishwa kwa Obama


Mara baada ya kukabiliana na matatizo hayo aliingia vitani kupitisha mpango wa mageuzi ya huduma za afya mhadhiri wa chuo kikuu cha Florida Charles Bwenge anasema hiyo ndio ushindi wake mkubwa wa masuala ya kijami.

“Marais walomtangulia walishindwa lakini alifanikiwa na hapo kubadilisha kabisa muelekeo wa siasa hapa Marekani, kwani kulijitokeza wapinzani wakuu wa mrengo wa kulia wenye siasa kali wanaojulikana kama The Tea Party.”

Mabadiliko hayo yaliweza kuonekana kwa chama cha Republican kluchukuwa udhibiti wa Baraza la Wawakilishi bungeni na kuongeza viti katika baraza la Senet. Mabadiliko hayo yaliyotokea kati kati ya mhula wake wa kwanza yalimpelekea Obama kushindwa kupitisha miswada na mapendekezo hayo kuanzisha mvutano mpya wa kisiasa Washington.