Muhtasari wa Habari Mbalimbali za Dunia

Rais wa Marekani Donald Trump, kulia, na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakiwa White House Jumatano Novemba 13, 2019.(AP Photo/ Evan Vucci)

Marais waeleza changamoto zinazozikabili Marekani na Uturuki  Marais hao wawili Donald Trump na Recep Tayyip Erdogan, walielezea mazungumzo yao huko White house kuwa yalikuwa na tija na ya ukweli. 

Ununuzi wa Uturuki wa silaha za kijeshi kutoka Russia kama vile S-400 kunapelekea changamoto kubwa sana kwetu Rais Trump alikiri katika mkutano na wana habari akiwa pamoja na rais Erdogan.

Ni matumaini yetu kuwa tutaweza kusuluhisha hali hiyo aliongeza rais Trump.

Islamic Jihad na Israel zafikia makubaliano

Kundi la wanamgambo wa kipalestina, Islamic Jihad limesema Alhamisi limesitisha mashambulizi kwa Israel, baada ya pande zote mbili kufikia mkubaliano yaliosimamiwa na Misri.

Msemaji wa kundi hilo amesema sitisho hilo limeanza rasmi hii leo asubuhi ikiwa ni pamoja na Israel kukubali masharti kadhaa pamoja na kuacha kuwalenga na kuuwa viongozi wa kundi hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Katz aliiambia radio ya jeshi kwamba majeshi ya Israel yatasitisha mashambulizi mengine kama ikiwa wapalestina nao watatulia. Lakini alikanusha juu ya mabadiliko katika sera ya Isrel kwamba haitasita kushambulia yeyote ambaye ana nia ya kuwaumiza.

Maadnamano : Chuo Kikuu cha Hong Kong chalazimika kufungwa

Chuo kimoja huko Hong Kong kimeamua kufunga milango yake kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na maandamano ya kuipinga serikali yanayoendelea kwa siku ya nne mfululizo hii leo.

Chuo kikuu cha China na vyuo vingine vimegeuzwa kuwa ngome za kujificha huku wanafunzi waandamanaji wakiweka vizuizi barabarani ili kuzuia polisi ambao wamejaribu kuingia vyuoni humo wiki hii.

Polisi wametumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kwa waandamanaji hao ambao nao wamejibu kwa kurusha matofali na mabomu ya gesi. Wanafunzi katika chuo kikuu kimoja waliamua hadi kutumia mishale kujibu mashambulizi ya polisi hao.

Chanjo mpya ya Ebola yazinduliwa DRC

Maafisa wa afya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezindua rasmi chanjo mpya ya Ebola iliyotenegenezwa na kampuni ya Johnson & Johnson, shirika la madaktari wasio na mipaka Medicines Sans Frontia -MSF limeeleza leo alhamisi ili kusaidia kupambana na mlipuko wa pili mbaya wa ugonjwa huo duniani.

Vifaa vipya ikiwa ni pamoja na chanjo, vimesaidia kudhibiti mlipuko huo ambao ni wa pili kwa ukubwa ukiacha ule wa mwaka 2013-2016 wa Afrika magharibi ambao uliuwa zaidi ya watu 11,300 licha ya kutoaminiana kwa umma na mizozo iliyoathiri mapambano na ugonjwa huo katika baadhi ya sehemu.

Chanjo hiyo ambayo imepita kwenye majaribio lakini haijawajahi kutumika katika uhalisia itawafikia watu wapatao 50,000 mjini Goma mji ulio na watu milioni mbili unaopaka na Rwanda Shirika la MSF limeeleza katika taarifa yake.