Muasisi wa chama Inkatha Freedom Mangosuthu Buthelezi afariki Afrika Kusini

Mwanasiasa mwenye utata wa Afrika Kusini na kiongozi wa kimila wa kabila kubwa la Wazulu wa Afrika Kusini, Prince Mangosuthu Buthelezi, wakati wa uhai wake akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni Machi 26, 2009.

Mangosuthu Buthelezi, mwanasiasa mkongwe wa Afrika Kusini, mwana mfalme wa Kizulu na mtu mwenye utata wakati wa mapambano ya ukombozi wa ubaguzi wa rangi amefariki dunia, ofisi ya rais ilisema leo Jumamosi. Alikuwa na umri wa miaka 95.

Muasisi huyo wa chama cha Inkatha Freedom alihudumu kwa mihula miwili kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi katika serikali ya baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika na chama tawala cha African National Congress –ANC mwaka 1994 kuchukua utawala.

"Nina masikitiko makubwa kutangaza kifo cha Prince Mangosuthu Buthelezi wa KwaPhindangene, Waziri Mkuu wa Jadi kwa ufalme na kabila la Wazulu na mwanzilishi na Rais Mstaafu wa chama cha Inkatha Freedom," Rais Cyril Ramaphosa alisema katika taarifa yake.