Raphael Samuel, mwenye umri wa miaka 27, ambaye ni raia wa India, anasema yalikuwa makosa makubwa kwa wazazi wake kumzaa bila ya idhini ya maoja kwa moja kutoka kwake.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Kanak la nchini India, Samwel amesema hata ingawa anafahamu kwamba haiwezekani kwa mtu kupeana idhini ya kuzaliwa, anashangaa ni kwa nini watu huzaliwa bila yao kueleza azma au nia ya kuishi maisha hapa duniani.
Samwel amesema anawasiliana kwa karibu sana na mawakili wake ambao, alieleza, hi karibuni watawasilisha kesi hiyo kwa msingi kwamba hafai kuendelea kupata mateso anyoyapoitia hapa duniani kwa sababu haukuwa uamuzi wake kuzaliwa.
Lakini ingawa suala kama hilo linaweza kuzua mtafaruku kwa familia nyingi, wazazi wa Samuel, ambao wote wawili ni mawakili, hawaonekani kubabaishwa na mpango wa mwanao kuwapeleka mahakamani.
Sikiliza:
Your browser doesn’t support HTML5
"Itakuwa vigumu sana kwao. Wamesema hata kama wewe ni mtoto wetu, na unatupenda na tunakupenda, tutakushinda mahakamani,' alisema Samuel.
"Mimi nataka iwe kesi yenye haki, ili umuhimu wa kauli yangu uonekane," aliongeza.
Kavita Karnad, ambaye ndiye mamaye Samuel amesema yuko tayari kukubali kwamba alifanya makosa kumzaa samwel iwapo mlalamishi ataishawishi mahakama.
Samwel anasema kwamba anaamini dunia hii bila wanadamu ingekuwa pahali pema kwa viumbe vingine, ikiwa ni pamoja na mimea.
Ingawa mipango yake hiyo imewashangaza watu wengi, kuna baadhi ambao wanasema kwamba anahitaji kupelekwa hospitali ili kupimwa akili, kwani, wanasema, huenda ana dalili zinazopelekea watu kujitoa uhai.
Tukitoka India, tupige kiguu na njia hadi barani Afrika, ambako vituko haviadimiki.
Mtu mmoja anashikiliwa kwenye kituo cha polisi mjini Athi River nchini Kenya, baada ya kukamatwa kwa shutuma zisizo za kawaida.
Moses Opanga, ambaye alikuwa amewaambia majirani zake kwamba mama yake alikuwa amekufa, alikamatwa baada ya kile polisi wanasema ni kubainika kwamba alikuwa amewatapeli majirani na waumini wenzake..
Majirani wamekiambia kituo cha televisheni cha NTV, kinachopeperusha matangazo yake kutoka mjini Nairobi, kwamba mtu huyo aliokota Zaidi ya shilingi elfu sita kama mchango kutoka kwao, lakini walipofika katika kijiji ambako walitarajia kumzika mamake mshukiwa, waligundua kwamba mamake hakuwa amekufa.
Majirani hao walikuwa wamesafiri kwa takriban kilomita 400 mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya lakini mtu huyo alitoroka na kuwaacha vinywa wazi.
Habari njema ni kwamba, mamake mshukiwa huyo bado yu hai licha ya kwamba hata naye alistaajabishwa mno na yale aliyoyafanya mtoto wake.