Mto mpya wazuka kaskazini mwa Los Angeles

  • VOA News

Picha ya awali ya helikopta ya moto katika Kaunti ya San Diego, California. Januari 21, 2025.

Mamlaka za California Jumatano zimetoa amri ya watu kuondoka kwenye maeneo ya ndani baada ya moto mpya  kuzuka ukiwa na upepo mkali kwenye milima iliyopo kasakzini mwa Los Angeles.

Moto huo wa Hughes uliyozuka Jumatano jioni na kisha kuenena kwa haraka kwenye mamia ya hekari za miti na majani ulizua moshi mwingi karibu na ziwa Castaic.

Moto huo umekuja wakati eneo kubwa la kusini mwa California lililochomeka vibaya hivi karibuni, likitarajiwa kupata mvua zinazohitajika sana mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo kuna hatari kwamba hata mvua usiyo mwingi unaweza kuzua changamoto kubwa kama kuenea kwa majivu yenye sumu. Wakati huo huo ilani ya hatari ya moto itaendelea kuwepo California hadi Alhamisi.