Marekani yatoa msaada wa kupambana na uasi Msumbiji

Wanajeshi wa Msumbiji wakifanya doria mitaani kufuatia mashambulizi yalioshukiwa kutoka kwa kundi la wenye msimamo mkali wa kiislam.

Afisa wa juu wa kupambana na ugaidi wa Marekani ameelezea wasiwasi wake juu ya kuzorota kwa hali nchini Msumbiji, ambapo kundi linaloshirikiana na Islamic State limeteka eneo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Lakini Balozi Nathan Sales anasema suluhisho la kijeshi sio jibu.

Kwa miaka mitatu, eneo la kaskazini mwa Msumbiji limekuwa ni kitovu cha shughuli na kikundi cha wanamgambo wa Kiislam wenye msimamo mkali. Mashambulizi yao yamesababisha kupoteza makazi kwa zaidi ya watu 400,000 na vifo vya zaidi ya wengine 2,000 katika mkoa wa Cabo Delgado.

Lakini, kama afisa mkuu wa Marekani wa kukabiliana na ugaidi anavyosema, mzozo huu unaathiri zaidi si kona moja tu ya kijiji cha taifa moja la Kusini mwa Afrika. Mzozo huo umeenea hivi karibuni katika nchi jirani ya Tanzania, na kuongeza uwezo wa kuingiza kanda hiyo kwenye kutokuwa na uthabiti na kulipa nguvu kundi lililo na uhusiano na Islamic State.

Suluhisho la kijeshi halitoshi-Balozi Sales

Balozi Nathan Sales, mratibu wa Marekani wa kukabiliana na ugaidi, hivi karibuni alitembelea Msumbiji na Afrika Kusini kuona jinsi Marekani inavyoweza kusaidia, katika hatua za “kuzuia, kuharibu, na kushinda” harakati inayoongezeka. Kwa hali ngumu,kiasi hiki alisema, suluhisho la kijeshi halitoshi.

Alizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne kwa njia ya simu kutoka Washington.

“Mbali na changamoto za kiusalama zinazosababishwa na watendaji wa ISIS huko, pia tuna matokeo ambayo tunaomba yasije kutokea kwa mtazamo wa kibinadamu, unajua maelfu ya raia wa Msumbiji wanaokimbia vurugu. Na kwa hivyo sehemu ya majibu inapaswa kujumuisha kukidhi hitaji hilo la kibinadamu. Tunapaswa kudhibiti hali ya usalama ili watu wajisikie raha na salama kurudi majumbani mwao, kurudi kwenye maisha yao.”alisema balozi Sales.

Alex Vines, mkurugenzi wa mpango wa Afrika huko Chatham House, anasema kuna sababu kadhaa ambazo ulimwengu unatilia maanani kona hii ndogo ya Afrika. Moja, Cabo Delgado ina amana kubwa ya mafuta na gesi ambayo haijaguswa inakadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 60. Kukosekana kwa utulivu kumezuia eneo hilo kuendelezwa.

Na anaongeza kwamba kundi la wapiganaji linazidi kuwa na ujasiri likisaidiwa na kutofaulu kwa serikali ya Msumbiji.

“Kwa hivyo kuna malalamiko ya ndani, kuna kufadhaishwa kweli kwamba serikali ya Msumbiji, na chama cha serikali hiyo haijasaidia , Kwa hivyo, vijana walionyimwa haki wamekatishwa tamaa. Na nadhani pia athari za kimbunga hicho mwaka jana kule mbali kaskazini kwa hivyo Kimbunga Kenneth, na majibu duni ya kibinadamu pia yalisababisha watu kuwa na huruma kwa uasi huu.” Alisema Vines.

Kwa hivyo ni nini mpango wa Marekani? Juu ya hayo, Sales hakuwa wazi.

Marekani ndio nguvu pekee ya nje inayojaribu kuingilia kati. Wiki hii, Papa Francis alitoa dola 121,000 kusaidia waathiriwa wa mashambulizi ya wanamgambo huko Cabo Delgado. Fedha hizo zitatumika kujenga vituo vya afya kwa wale waliokimbia makazi yao.

Na, Vines alibaini, mamluki na kikundi cha Wagner walifika Msumbiji mwishoni mwa 2019 ili kusaidia vikosi vya usalama vya Msumbiji. Maafisa wakuu wa jeshi la Marekani wameunga mkono wachambuzi ambao wanaamini kuwa Kikundi cha Wagner kina mahusiano ya karibu na Kremlin, shtaka ambalo maafisa wa Russia wamekanusha.

Msumbiji pia imekuwa ikifanya mazungumzo na Uingereza na nchi jirani ya Afrika Kusini kwa msaada katika kupambana na uasi unaoongezeka.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC.