Msumbiji na Malawi watathmini gharama ya Kimbunga Freddy

Mtu mmoja akiondoka kwenye majengo yaliyoharibiwa na Kimbunga Freddy huko Chilobwe, Blantyre, Malawi, Machi 13, 2023. REUTERS/Eldson Chagara.

Msumbiji na Malawi siku ya Jumatatu walikuwa wakitathmini gharama ya Kimbunga Freddy, ambacho kiliua zaidi ya watu 100, kujeruhi watu wengi na kuacha njia ya uharibifu wakati kilipokumba kusini mwa Afrika kwa mara ya pili katika mwezi mmoja mwishoni mwa juma.

Freddy ni mojawapo ya dhoruba kali zaidi kuwahi kurekodiwa katika upande wa kusini mwa dunia na kinaweza kuwa kimbunga cha muda mrefu zaidi cha kitropiki, kulingana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Kilikumba eneo la kati la Msumbiji siku ya Jumamosi, na kuezua paa za majengo na kuleta mafuriko kuzunguka bandari ya Quelimane, kabla ya kuingia ndani kuelekea Malawi na mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya ardhi.

Kiwango kamili cha uharibifu na upotezaji wa maisha nchini Msumbiji bado hakijabainika, kwani umeme na simu zilikatika katika baadhi ya maeneo yalioathiriwa.

Dharuba hiyo imeua watu 99 nchini Malawi, wakiwemo 85 katika kituo kikuu cha kibiashara cha Blantyre, alisema kamishna wa Idara ya Masuala ya Kukabiliana na Maafa, Charles Kalemba, katika mkutano na waandishi wa habari