Mshindi wa tuzo ya nobeli akosoa mtandao wa Facebook

In this photo provided by the Rappler, Rappler CEO and Executive Editor Maria Ressa reacts after hearing she won the Nobel Peace Prize, inside her home in Taguig, Metro Manila, Philippines, Oct. 8, 2021.

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Ressa alitumia umaarufu wake wa hivi karibuni kukosoa mtandao wa Facebook kuwa tishio kwa demokrasia

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Ressa alitumia umaarufu wake wa hivi karibuni kukosoa mtandao wa Facebook kuwa tishio kwa demokrasia, akisema mtandao huo mkubwa wa kijamii unashindwa kulinda dhidi ya kuenea kwa chuki na habari mbaya na ni ya upendeleo dhidi ya ukweli.

Mwanahabari huyo mkongwe na mkuu wa tovuti ya habari ya Ufilipino Rappler aliiambia Reuters katika mahojiano baada ya kushinda tuzo hiyo kwamba algorithms za Facebook zinatoa kipaumbele kuenea kwa uwongo uliojaa hasira na chuki juu ya ukweli.

Maoni yake yanaongeza mkusanyiko wa shinikizo la hivi karibuni kwenye Facebook, inayotumiwa na zaidi ya watu bilioni 3 duniani, ambayo mfanyakazi wake wa zamani aliyegeuka mtoa habari wa siri akiituhumu kampuni hiyo kwa kutafuta faida badala ya haja ya kuzuia matamshi ya chuki na habari potofu. Facebook inakanusha makosa yoyote.

Alipotafutwa kwa ajili ya maoni juu ya matamshi ya Ressa, msemaji wa Facebook alisema mtandao huo mkubwa wa kijamii unaendelea kuwekeza sana ili kuondoa na kupunguza mwonekano wa yaliyomo hatari.

"Tunaamini katika uhuru wa vyombo vya habari na tunaunga mkono mashirika ya habari na waandishi wa habari ulimwenguni pote wanapoendelea na kazi yao muhimu," msemaji huyo aliongeza.