Msemaji wa jeshi la polisi Uganda auawa

Shambulizi la msemaji wa Jeshi la polisi Uganda

Watu wasiojulikana wamempiga risasi na kumuuwa msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uganda shambulizi hilo lilitokea Ijumaa wakati kamanda huyo anaondoka nyumbani kwake Kulambiri, Kisaasi kaskazini mashariki mwa makao makuu ya Uganda, Kampala.

Taarifa hizo zinasema kuwa walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa katika tukio hilo.

Marehemu Felix Kaweesi alipigwa risasi siku moja baada ya kuwa mstari wa mbele kukanusha taarifa za shirika la haki za binadamu Human Rights Watch zilizokuwa zinaibana serikali kufanyika uchunguzi juu ya mauaji ya Kasese.