Warepublikan ambao walikutana kwa faragha Jumanne jioni, walimchagua Mike Johnson kuwa mgombea wa karibuni wa nafasi ya spika wa Baraza la Wawakilishi, ni mgombea wanne tangu Mwakilishi Kevin McCarthy alipoondolewa katika nafasi hiyo.
Johnson ni mwakilishi kutoka jimbo la Louisiana ambaye aliwahamasisha Warepublikan kuuunga mkono juhudi za Rais wa zamani Donald Trump kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020.
Alipata kura 128 Jumanne usiku na kuwashinda wagombea wengine. McCarthy, ambaye hakuwa mgombea aliyechaguliwa, alichukua nafasi ya pili kwa kupata kura 43.
Haiko bayana iwapo Johnson ataweza kupata uungaji mkono wa Warepublikan wengi katika Baraza hilo, kitu ambacho wagombea watatu waliotangulia wakiwania kuchukua nafasi ya McCarthy walishindwa kupata uungaji mkono huo.
Warepublikan wana wingi mdogo wa wawakilishi 221dhidi ya 212, na Wademokrat walimuunga mkono kiongozi wa Wademokrat katika Baraza hilo Hakeem Jeffries, mgombea yoyote wa Republikan anaweza kushindwa tu kura chache za Warepublikan na bado akapata wingi ulio na idadi inayohitajika kushinda nafasi ya uspika.
Warepublikan walimteua Johnson baada ya mgombea mwingine, Mwakilishi Tom Emmer, kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho mapema Jumanne.
Kiasi cha Warepublikan 20 katika Baraza la Wawakilishi walisema hawatamchagua Emmer, na hivyo kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.