Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mpango huo sasa umeongezewa muda lakini haikusemwa ni kwa kiwango gani.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema kwamba mpango wa nafaka wa black Sea pamoja na mkakati wa bidhaa za chakula za Russia ni muhimu kwa usalama wa chakula duniani hasa kwa mataifa yanayo endelea.
Alisema hayo katika taarifa ambapo ameongeza kwamba wanaamini zaidi katika makubaliano hayo na wanatoa mwito kwa pande zote kuongeza juhudi za kutekeleza waliyokubaliana kikamilifu.
Kwa mujibu wa yale waliyokubaliana, kuongezewa muda kwa mpango huo kunapaswa kuwa kwa siku 120, lakini Russia imekuwa ikitaka uongezwa kwa nusu ya muda huo.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, pamoja na Umoja wa Mataifa waliofanikisha mpango huo, wamethibitisha kuongezwa muda lakini hawakueleza ni kwa muda gani.
Waziri wa miundombinu wa Russia kupitia ujumbe wa Twitter amesema umeongezwa kwa siku zote 120.