Uingereza imefikia makubaliano ya paundi milioni 120 (dola milioni 148) na Rwanda kutuma baadhi ya wahamiaji, ambao walivuka kinyume cha sheria kupitia eneo dogo la bahari kwa kutumia boti ndogo ndogo kutoka Ulaya, ili kuishi katika nchi hiyo ya Afrika isiyo na bandari.
Mpango huo umewatia hofu wapinzani wa kisiasa, mashirika ya misaada na viongozi wa makanisa wanaosema kuwa ni kinyume cha utu. Mkuu wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa aliliita ni janga, uongozi mzima wa Kanisa la Uingereza ulishutumu kama sera zisizo na maadili zinazoaibisha Uingereza.
Serikali inasema mkakati wa kuwafurusha unahitajika ili kukomesha mtiririko wa wahamiaji wanaohatarisha maisha yao katika vivuko vya baharini na kuvunja mitandao ya magendo ya watu.