Mpalestina ashambuliwa kituo cha jeshi la Israel

Mshambuliaji wa Kipalestina alifyatua risasi katika kituo cha ukaguzi cha jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu siku ya Jumamosi kabla ya kupigwa risasi na kuuawa, polisi wa Israel wamesema.

Hili ni tukio la hivi karibuni kabisa katika miezi kadhaa ya ghasia zinazozidi kuongezeka.

Mpiganaji huyo wa kipalestina alikaribia wanajeshi wa Israel waliokuwa kwenye kizuizi cha Qalandiya nje ya Jerusalem, mapema asubuhi, akachomoa bunduki aina ya M16 na kufyatua risasi, polisi wa Israel wamesema.

Vikosi vya usalama vya Israel vimesema vilimpiga risasi na kumuua mshukiwa huyo.

Kwa mujibu wa idara ya huduma ya uokozi ya Israeli, walinzi wawili wa usalama wenye umri wa miaka 20 walilazwa hospitali wakiwa na majeraha madogo, huku mmoja kutokana na risasi.

Hakukuwa na taarifa za haraka kuhusu wale walio husika katika shambulizi hilo. Tukio hilo linaendeleza wiki ya umwagaji damu katika Ukingo wa Magharibi ambapo Wapalestina 15 na Waisrael wanne wameuwawa.