Katika saa chache , moto ulisambaa kufika hadi theluthi mbili kwa ukubwa kuliko ule moto wa Eaton moja ya mioto mkubwa ulioharibu maeneo kadhaa ya mji.
Mkuu wa polisi wa kaunti ya Los Angeles alisema kwamba watu 31,000 walitakiwa kuhama na wengine elfu 23 walipewa onyo la kuondoka kutoka makazi yao.
Moto mpya umesababisha ugumu kwa wafanyakazi wa zimamoto ambao wamekaribia kuudhibiti moto mkubwa katika maeneo mengine mawili ya eneo hilo .
Idara ya misitu ya California na udhibiti wa moto imesema takriban wafanyakazi 1,100 wa zimamoto wamepelekwa kusini mwa California kupambana na moto uliokuwa unaendelea kwa kasi.