Mohamed Morsi ahukumiwa miaka 20 gerezani

Rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi akiwa kwenye chumba cha mahakama mjini Cairo, Nov. 3, 2014.

Mahakama moja nchini Misri Jumanne ilimhukumu Rais wa zamani Mohamed Morsi kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji katika mwaka 2012.

Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mkazi mmoja wa Cairo, Abdirazak Ninyigaba na kwanza ilimuuliza wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood cha bwana Morsi.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano ya VOA na Abdirazak Ninyigaba mkazi wa Cairo, Misri

Bwana Morsi aliepuka uwezekano wa adhabu ya kifo wakati mahakama ilipotoa hukumu kwamba yeye na viongozi 12 wengine wa kundi la Muslim Brotherhood pamoja na wafuasi wa kundi hilo walikutwa na hatia ya kuchochea ghasia, lakini sio mauaji.

Wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood

Mashtaka hayo yanahusiana na mapambano nje ya ikulu ya rais ambayo yalianzishwa na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood la bwana Morsi lilipowashambulia waandamanaji ambao walikuwa wakilalamika dhidi ya amri ya rais inayodai kwamba maamuzi yake hayawezi kuingiliwa na mahakama.

Bwana Morsi, Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo aliingia madarakani takribani miaka minne iliyopita akiahidi kuleta mabadiliko nchini Misri baada ya uwasi wa wananchi ulioangusha utawala wa kiongozi wa muda mrefu nchini Misri wa bwana Hosni Mubarak.