Kutoka Afrika Mashariki, Mohammed Dewji, maarufu Mo, mfanyabiashara tajika na raia wa Tanzania ametajwa kwkama miongoni mwa mabilionea 20 wa bara hilo, akishikila nafasi ya 16.
Hata hivyo, kwa mujibu wa jarida hilo, utajiri wa bilionea huyo, ambaye anamiliki kilabu cha soka cha Simba, umedaiwa kupungua hadi dola bilioni 1.6.
Mo aligonga vichwa vya habari mwezi Oktoba mwaka 2018 baada ya kutekwa nyara na baadaye kuachiliwa baada ya siku kumi, katika kile kilichotajwa na wachambuzi kama kisa kisicho cha kawaida.
Kufikia sasa, hajajulikana bayana ni nani walimteka nyara mjasiriamali huyo au ni kwa nini, huku maafisa wa serikali ya Tanzania wakisisitiza mara kwa mara kwamba bado wanaendelea na uchunguzi dhidi ya kisa hicho. Mwezi Oktoba 2018, watu watatu walikamatwa kuhusiana na kesi hiyo.
Mo alizaliwa tarehe 8 Mei mwaka 1975, mjini Ipembe, mkoa wa Singida, akiwa pili miongoni mwa watoto sita wa Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji.
Alisomea chuo kikuu cha Gerogetown jijini Washington DC na kuhitimu mwaka 1998 na shahada katika biashara ya kimataifa na fedha na masuala pia ya dini.
Baada ya hapo, alirejea Tanzania na kuanza kushiriki katika usimamizi wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Baadaye alipanua wigo wake na kuanzisha makampuni mbalimbali, hali iliyomfanya mmoja wa Watanzania maarufu zaidi.
Tukirejelea ripoti hiyo mpya ya Forbes, Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara za aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uzalishaji na uuzaji wa saruji, sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1.
Dangote anafuatiwa na mfanyabiashara wa Misri Nassef Sawaris, ambaye aliongeza utajiri wake kutoka dola bilioni 6.3, alizokuwa nazo mwaka uliopita, hadi dola bilioni nane.
Isabel dos Santos mwenye utajiri wa dola bilioni 2.2, ameendelea kushikilia taji la mwanamke tajiri Zaidi barani Afrika.
Inaaminika kwamba Bi Dos Santos alijipatia utajiri wake wakati babake alipokuwa rais ambapo alianza kumiliki hisa katika makampuni mengi ya Angola pamoja na benki.
wa aliyekuwa rais wa Angola Isabel dos Santos ni miongoni
Wakati huo huo, Katika orodha ya watu wanne matajiri zaidi duniani, Bernard Arnault, sasa ndiye mtu tajiri zaidi duniani akiwa na mali yenye thamani ya dola billioni 116.5.
Bernard anamiliki kamapuni ya mitindo ya Louis Vuitton na Sephora.
Jeff Bezos, kutoka Marekani, anayemiliki mali yenye thamani ya dola bilioni 115.6 alitangazwa kuwa mtu wa pili kwa utajiri zaidi duniani, huku nafasi ya tatu ikienda kwa mjasiriamali tajika, Bill Gates, mwenye mali yenye thamani dola bilioni 110.6.