Mlipuko waua watu 4 na kujeruhi kadhaa Uturuki

Polisi na wafanyakazi wa huduma ya dharura wakiwa katika sehemu kulipotokea mlipuko katika barabara ya Istiklala, Istanbul, Uturuki Nov 13, 2022

Watu wanne wamefariki na zaidi ya 38 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye barabara yenye shughuli nyingi katikati mwa Istanbul.

Kwa kawaida, sehemu ambapo mlipuko umetokea katika wilaya ya Beyoglu, ina idadi kubwa ya watu ikiwemo wateja, watalii na watu kutoka familia wanaofanya matembezi.

Shirika la habari la serikali ya Uturuki TRT limeripoti kwamba maafisa wa usalama wanaendelea kuchunguza kilichotokea.

Gavana wa IstanbuliAli Yerlikaya, ameandika ujumbe wa twitter kwamba mlipuko umetokea saa kumi alasiri.