Mlipuko katika mkoa wa magharibi mwa Ghana uliotokea Alhamisi, umechoma mamia ya majengo, na kuuwa watu kwa idadi ambayo haijafahamika baada ya lori la vilipuzi vya mgodi wa dhabahu kugongana na pikipiki.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba video ambazo hazikuweza kuthibitishwa za vyombo vya habari vya nchini humo zimeonyesha eneo la mlipuko ambako majengo yameharibika yakiwa yamefunikwa na mbao, matofali na vyuma.
Video moja imeonyesha maiti mbili zikiwa ardhini na kufunikwa na vumbi. Naibu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya taifa ya kushughulikia majanga, Seji Saji amesema kwamba majengo 500 yameharibiwa.
Afisa wa idara ya kikanda ya dharura amevieleza vyombo vya habari vya Ghana kwamba maiti 10 tayari zimepatikana. Polisi wamesema kwamba miji ya karibu imeombwa kuacha wazi sehemu za umma ikijumuisha madarasa na makanisa ili walionusurika wapatiwe hifadhi