Takriban watu wanane waliuawa katika mji mkuu wa Somalia Alhamis wakati wanamgambo wa kiislam walipofanya shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya msafara wa usalama wa Umoja wa Mataifa kwa kutumia gari lililojaa vilipuzi, maafisa na mashahidi walisema.
Kundi la kiislam la al Shabaab lilidai kuhusika na mlipuko huo mkubwa uliouitikisha Mogadishu na kujeruhi takribani watu 23 wakiwemo wanafunzi wa shule huku moshi mkubwa ukiw aumetanda angani mjini humo. Milio ya risasi ilisikika karibu na eneo la tukio, mashahidi walisema.
Haijabainika mara moja ikiwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, walikuwa miongoni mwa waliouawa au kujeruhiwa katika mlipuko huo mkubwa uliolenga msafasra wa Umoja wa Mataifa ulipokuwa ukipita karibu na eneo la shule. Maafisa wa Umoja wa Mataifa hawakujibu mara moja, kutoa maoni yao.
Tulihesabu watu wanane waliokufa na wengine 17 wakiwemo wanafunzi 13 waliojeruhiwa, msemaji wa polisi Abdifatah Aden Hassan, aliwaambia waandishi wa habari. Alisema mashambulizi ya kujitoa mhanga katika gari aina ya SUV iliyojaa vilipuzi yalilenga msafara wa usalama wa Umoja wa Mataifa.
Gari la kubeba wagonjwa katika kituo cha Aamin liliwahamisha angalau watu 23 waliojeruhiwa katika mlipuko huo Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa huduma wa kituo hicho aliliambia shirika la habari la Reuters.