Mlipuko katika kinu cha mafuta kisicho rasmi kusini mwa Nigeria umeua takriban watu 80, idara ya huduma za dharura ilieleza Jumapili.
Mlipuko huo ulitokea Ijumaa usiku katika eneo lisilo halali kati ya majimbo ya kusini ya mafuta ya Rivers na Imo, polisi walisema.
“Tulipata takriban miili 80 iliyoungua vibaya kwenye eneo la tukio” Ifeanyi Nnaji wa Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Dharura (NEMA) katika eneo hilo, aliiambia AFP, na kuongeza kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi.
"Tuligundua miili mingi iko kwenye vichaka na misitu iliyo karibu huku baadhi ya waendeshaji haramu na wafadhili wao wakitoroka kutafuta usalama."aliongeza.