Kufuatia kujiondoa kwa Rais Joe Biden katika kinyang’anyiro cha urais, mtizamo wa Chama cha Demokratik umejikita katika mkutano mkuu wa uteuzi wa wagombea. Wakati hatua ya Biden kujitoa dakika za mwisho katika ushindani umepelekea wengi kuamini kuwa wanaweza kushuhudia mkutano wa kwanza wa wazi kuwahi kufanyika kwa miongo kadhaa, lakini badala yake, wajumbe mara moja walijitokeza kumuunga mkono Makamu wa Rais Kamala Harris.
Mikutano ya wazi imekuwa ni sehemu ya muundo wa kisiasa katika sehemu kubwa ya historia ya Marekani.