Mkutano wa masuala ya Nyuklia kufanyika Washington

Rais wa Marekani Barack Obama

Ujumbe kutoka mataifa 50 unawasili kwa ajili ya mkutano wa siku mbili ambao utaangalia namna ya kuhakikisha mali ghafi za kutengenezea silaha za nyuklia hazifiki mikononi mwa magaidi ama watu wenye nia ya kufanya ughalifu.

Rais wa Marekani, Barack Obama, atakuwa mwenyeji wa mkutano wa nne na wa mwisho wa usalama wa nyuklia mjini Washington unaoanza Alhamisi.

Ujumbe kutoka mataifa 50 unawasili kwa ajili ya mkutano wa siku mbili ambao utaangalia namna ya kuhakikisha mali ghafi za kutengenezea silaha za nyuklia hazifiki mikononi mwa magaidi ama watu wenye nia ya kufanya ughalifu.

Marekani inasema imesikitishwa kwamba Russia imeamua kutoshiriki mkutano huo. Katika mkutano huo Rais Obama atakutana na kitengo cha uangalizi wa nyuklia cha Umoja wa Mataifa cha ‘International Atomic Energy Agency Interpol” na makundi mengine kujadili kuboresha usalama katika nyuklia.