Akifungua mkutano wa 18 mjini Vienna Uswisi, Dk Sidibe alisema mkutano wa Vienna una umuhimu mkubwa kwa vile unaofanyika miaka 10 baada ya mkutano kama huu huko Durban, Afrika Kusini ambao ulileta mabadiliko makubwa katika matibabu ya ukimwi kote duniani ni miaka 5 tu kabla ya kufikia tarehe ya mwisho kabla ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya Milenia MDGs.
Akifungua mkutano huo, Jumapili Bw Sidibe amesema mkutano huu wa Vienna utatahmini maendeleo muhimu yaliyopatikana, katika miaka 20 iliyopita na kutafakari juu ya changa moto zilziopo na njia ya kuendelea mbele katika vita dhidi ya janga hili.
Na kuweza kufikia malengo hayo UNAIDS imeangaza mkakati mpya wa kupambana na HIV Ukimwi unaojulikana kama Tiba 2.0. Dk Sidibe anasema mkakati mpya unalengo la kupunguza gharama za matibabu na madawa, na wakati huo kuimarisha juhudi za watu kujingina kutokana na uambukizaji wa hiv. Zaidi ya hayo mkutano huu utazungumzia kuimarishwa kwa aki za binadamu kwa waathiriwa, kutokana na kauli mbiyu ya mkutano “Haki Sasa-Haki Hapa”.
Akihutubia mkutano Jumatat asubuhi rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alitetea mkakati mpya wa rais Barack Obama, akisema ni kiongozi anaejaribu kutekeleza ahadi zake. Amesema kuhusiana na fedha alizoahidi kutoa kwa ajili ya kupambana na ukimwi haitounuka bali natokana na hali ya kiuchumi na sheria zinazopitishwa bungeni mnamo mwaka moja na nusu iliyopita katika juhudi zake za uufufua uchiumi dniani.
Mbali na majadiliano juu ya masuala ya HIV-Ukimwi, kuna maonesho, tamasha na mandamano ili kuhamasisha juu ya mauala mbali mbali yanaohusina na ukimwi.