Mkurugenzi wa CDC Marekani anasema virusi vya Delta vinasambaa haraka

Mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC) Marekani, Dr. Rochelle Walensky

Maafisa wa Washington, siku ya Alhamis waliwasihi watu kupata chanjo ya COVID ili kujilinda wenyewe kutokana na aina mpya ya virusi na kuzuia kuenea kwa maambukizi

Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Marekani, Rochelle Walensky, alisema Alhamis kwamba aina mpya ya virusi vya Corona vya Delta ambavyo vinasababisha COVID-19 ni "mojawapo ya virusi tunavyojua vinaambukiza kwenye mfumo wa kupumua ambavyo nimeshuhudia katika kazi yangu ya miaka 20".

Maafisa wa Washington siku ya Alhamis waliwasihi watu kupata chanjo ya COVID ili kujilinda wenyewe kutokana na aina mpya ya virusi na kuzuia kuenea kwa maambukizi.

Shirika la afya Duniani (WHO)

Wakati huo huo China haina furaha kwamba shirika la afya duniani (WHO) linataka kuendelea kuchunguza iwapo virusi vya Corona vilikimbia kutoka maabara huko Wuhan, na kupelekea janga la COVID-19 dunia nzima.

Naibu Waziri wa tume ya taifa ya afya nchini China, Zeng Yixin, alisema Alhamis kwamba pendekezo la WHO la kufungua tena uchunguzi wake juu ya uvujaji wa maabara ya China kama chanzo cha mlipuko wa ulimwengu lilikosa kuheshimu busara na mtazamo kuelekea sayansi. Alisema China haiwezi kukubali mpango kama huo.