Mkurugenzi mkuu wa kulinda mbuga asimamishwa kazi DRC

Ndovu wa Afrika kwenye picha ya maktaba

Wizara ya mazingira ya DRC imemsimamisha kazi mkurugenzi wa idara ya hifadhi yenye mamlaka ya kulinda mbuga za kitaifa za wanyamapori, zilizoorodheshwa na shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) kama turathi.

Wizara ya mazingira ya DRC, imemsimamisha kazi mkurugenzi wa idara ya hifadhi yenye mamlaka ya kulinda mbuga za kitaifa za wanyamapori, zilizoorodheshwa na shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) kama turathi.

, Hayo ni kwa mujibu wa barua rasmi iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa juma ingawa wizara hiyo haikutoa maelezo zaidi. Hata hivyo, afisa mwandamizi wa serikali amethibitisha kusimamishwa kazi kwa Cosma Wilungula ambaye ni mkurugenzi wa idara ya ICCN.

Afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa, amesema hatua hiyo huenda imechochewa na madai ya ubadhirifu wa fedha za kitalii kutoka Rwanda wakati wageni wakitembelea mbuga ya kitaifa ya Virunga ilioko mashariki mwa Congo.