Mkundi ya Kikurdi ya Syria yanaamini utwala mpya wa Trump utaendelea kuwaunga mkono

  • VOA News

Picha ya maktaba ya wapiganaji wa Kikurdi wa SDF nchini Syria.

Makundi ya Wakurdi nchini Syria yameelezea matumaini yao kwamba  Marekani itaendelea kuwaunga mkono wakati rais mpya Donald Trump anapoanza kuhudumu kwenye muhula wa pili.

Vikosi vya Kikurdi vya Demokratik, SDF, nchini Syria vimekuwa mshirika wa karibu wa Marekani kwenye vita dhidi ya kudi la kigaidi la Islamic State ambalo pia linajulikana kama ISIS. Vikosi hivyo vinashikilia sehemu kubwa ya Syria ambayo hapo nyuma ilikuwa chini ya udhibiti wa ISIS. Kamanda mkuu wa SDF Mazioum Abdi alikuwa miongoni mwa watu waliopongeza Trump baada ya kuapishwa kwake.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Syria wa muda mrefu wake rais Bashar al Assad mwezi uliyopita, vikosi vya Kikurdi vinavyoungwa mkono na Marekani vimekuwa vikishinikizwa na utawala mpya mjini Damascus, pamoja na Uturuki kuweka silaha chini.

Vikosi vinavyoungwa mkono na Uturuki pia vimekuwa vikizozana na SDF kwenye baadhi ya maeneo kaskazini mwa Syria. Uturuki inachukulia SDF kuwa sehemu ya chama cha wafanya kazi cha Kikurdi au PKK ambacho kimeordheshwa na Washington na Ankara kuwa la kigaidi.