Mke wa Rais Rawlings kwenye kinyan'ganyiro cha urais

Rais wa Ghana John Atta Mills(wa pili kulia) apata mpinzani ndani ya chama chake.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais anayetawala kukabiliwa na changamoto kutoka mwanachama wa chama tawala.

Mke wa rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings amesema atashindana na rais wa sasa katika uchaguzi wa awali wa chama tawala.

Nana Konadu Agyeman Rawlings alipeleka barua kwa katibu mkuu wa chama cha National Democratic Congress jana akisema anajiuzulu nafasi yake ya makamu wa mwenyekiti wa kwanza ili aweze kugombea nafasi ya rais wa chama chake.

Amesema atagombea uteuzi huo dhidi ya rais John Atta Mills katika uchaguzi wa awali wa July. Hii ni mara ya kwanza kwa rais anayetawala kukabiliwa na changamoto kutoka mwanachama wa chama tawala.

Tangazo hilo la mama wa kwanza wa zamani linaashiria mgawanyiko ndani ya chama tawala nchini humo.