Mkataba wa Russia na Korea Kaskazini unaweza kuwaunganisha Marekani na China

North Korea RussiaNorth Korea Russia Photo Gallery

Mkataba wa karibuni wa ulinzi kati ya Russia na Korea Kaskazini unaweza kutoa fursa ya kidiplomasia kwa Marekani na China kufanya kazi pamoja kwa ajili ya utulivu wa Peninsula ya Korea, suala ambalo lina maslahi kwa nchi zote mbili, baadhi ya wataalam wanasema.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Kurt Campbell, Jumatatu amesema kuwa China itakuwa na wasiwasi kuhusu kuimarishwa ushirikiano kati ya Russia na Korea Kaskazini, na kuongeza kuwa maafisa wa China wameonyesha hivyo katika baadhi ya mazungumzo yao na tunaona mvutano fulani unaohusishwa na mambo hayo.

Msemaji wa usalama wa taifa wa White House, John Kirby, amewaambia wanahabari baada ya mkutano wa Russia na Korea Kaskazini wiki iliyopita mjini Pyongyang kwamba wasiwasi wa makubaliano mapya ya ulinzi kati ya nchi hizo mbili utaelezwa na China.