Haiti ni nchi ambayo imekumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na mafaa ya majanga, maafisa wamesema Alhamisi. Daniel Foote aliteuliwa kwenye uadhifa huo mwezi Julai, kufuatia kuuawa kwa rais Jovenel Moise.
Hata kabla ya kufukuzwa wahamiaji hao kutoka mji mdogo wa Texas wa mpakani, Del Rio, mwanadiplomasia huyo anajulikana kama mtu aliyekerwa sana na kile alichoona kama ukosefu wa hatua za haraka kutoka Washington na uzembe katika juhudi za kuboresha hali nchini Haiti.
Foote alimuandikia waziri wa mambo ya nje Antony Blinken akimuelezea kwamba amejiuzulu mara moja, “kwa masikitiko makubwa na kuomba msamaha wale wanaotaka mabadiliko muhimu”.
Foote ameandika” sitahusishwa na uamuzi wa Marekani usiojali utu, uamzi usiokuwa na tija kuwarudisha Haiti maelfu ya wakimbizi wa Haiti na wahamiaji haramu, nchi ambako maafisa wa Marekani wanabaki ndani kulinda nyumba zao kwa sababu ya hatari inayosababishwa na magenge yenye silaha kwa maisha ya kila siku”.
Ameongeza kuwa “ mfumo wetu wa sera kwa Haiti bado una kasoro kubwa, na mapendekezo yangu ya sera yalipuuzwa na kutupiliwa mbali, au kuhaririwa na kutoa maelezo tofauti na yangu”.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imemkosoa Foote kwa kujiuzulu katika kipindi kigumu na imetupilia mbali madai kwamba mapendekezo yake ya sera yalipuuzwa.