Ni shambulio la pili baya katika siku za hivi karibuni.
Wapiganaji wa kijihadi walishambulia alfajiri, msemaji wa jeshi amesema katika taarifa.
“Afisa mmoja na wanajeshi wanne waliuawa na wanajeshi wengine wawili walijeruhiwa,” taarifa hiyo imesema na kuongeza kuwa wanajihadi saba waliuawa.
Hakuna aliyedai kufanya shambulio hilo la Jumatano, ambalo lilitangazwa na jeshi wakati rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi alikuwa akikutana na mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan.
Lakini shambulio hilo linafanyika siku nne baada ya shambulio la kuvizuia kwenye Peninsula ya Sinai lililodaiwa na kundi la Islamic State kuwauwa wanajeshi 11 wa Mistri, ikiwa mauaji makubwa kuwahi kutokea upande wa jeshi la Mistri kwa miaka mingi.
Peninsula ya Sinai imekuwa ikikabiliwa kwa zaidi ya muongo mmoja na uasi wa wanajihadi, ambao ulifikia kilele baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani mwenye itikadi kali za kiislamu Mohammed Morsi mwaka wa 2013.