Misri haitaruhusu tishio lolote kwa Somalia au usalama wake, Rais Abdel Fattah al-Sisi alisema Jumapili, kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya rais, baada ya Ethiopia kusema itafikiria kutambua madai ya uhuru wa Somaliland.
Akijaribu “kuingilia kipande cha ardhi” ilikudhibiti ni jambo ambalo hakuna atakayekubali, Sisi alisema katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud mjini Cairo.
Katika waraka wa maelewano uliotiwa saini Januari mosi Ethiopia ilisema itazingatia kutambua uhuru wa Somaliland ili kupata fursa ya kufika Bahari ya Sham.
Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka Somalia mwaka 1991 lakini haijapata kutambuliwa na nchi yoyote.