Zaidi ya watu 150 wauawa na wengi kujeruhiwa Brazzaville
Wanadiplomasia na maafisa wa serikali wanasema takriban watu 150 wakiwemo wafanyakazi wa China wameuwawa katika mfululizo wa milipuko katika Jamhuri ya Congo kwenye mji mkuu wa Brazzaville.
Maafisa wanasema msururu wa milipuko ulitokea kwenye ghala la kuhifadhia silaha karibu na ziwa Congo na kuutingisha mji huo Jumapili.
Afisa wa China kutoka ubalozi huko Brazzaville aliliambia shirika la habari la Beijing Xinhua kwamba takriban wafanyakazi wanne wa China ni miongoni mwa waliouwawa na dazani ya wengine kujeruhiwa. Haikufahamika mara moja kilichosababisha ghala hilo la silaha kulipuka.