Sehemu za kaskazini magharibi na zile za magharibi ni ndiyo zimekumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya vituo vya petroli katika mji mkuu wa Nairobi vinashindwa kuwauzia wenye magari mafuta kwasababu hawana mafuta.
Vyanzo vya habari vinasema kwamba uhaba wa mafuta unachangiwa na uagizaji mdogo wa bidhaa hiyo, kampuni za kuagiza mafuta zikihofia kwamba huenda zisipate faida kutokana na hatua ya serikali kupunguza bei ya bidhaa hiyo.
Lakini mamlaka ya kudhibithi bei ya mafuta nchini Kenya, imesema kwamba uhaba wa mafuta unatokana na changamoto za usafiri na kwamba zinafanya mazungumzo na kampuni za kuuza mafuta ili kupata suluhisho.
Kwa kawaida, serikali hutoa fidia kwa kampuni za kuuza mafuta ili kupunguza bei ya bidhaa hiyo, lakini wasafirishaji wa mafuta wanasema hawajalipwa kwa mda wa miezi minne sasa.
Lita milioni 380 za mafuta ya Petrol zinatumika kila mwezi nchini Kenya.