Miili zaidi ya 60 imeokolewa na chama cha hilali nyekundu cha Libya

Baadhi ya wahamiaji waliookolewa na makundi ya kutoa msaada wa dharura katika bahari ya Mediterranean. June 2018

Kundi hilo la kutoa msaada wa kibinadamu lilisema boti ilizama kaskazini ya mwambao wa mji wa Khoms uliopo kilomita 120 mashariki ya mji mkuu Tripoli nchini Libya ikiwa imebeba wahamiaji wapatao 350

Chama cha hilali nyekundu nchini Libya kiliokoa zaidi ya miili 60 kutoka ufukweni siku ya Ijumaa, siku moja baada ya boti iliyobeba wahamiaji wanaoelekea ulaya kuzama katika bahari ya Mediterranean.

Kundi hilo la kutoa msaada wa kibinadamu lilisema boti hiyo ilizama kaskazini ya mwambao wa mji wa Khoms uliopo kilomita 120 mashariki ya mji mkuu Tripoli. Boti ilikuwa imebeba wahamiaji wapatao 350.

Walinzi wa pwani wa Libya waliokoa darzeni ya miili ya wahamiaji wanaoelekea ulaya wakati operesheni ya utafutaji ilipoendelea hadi Ijumaa. Wahamiaji hao wanatoka katika mataifa ya Sudan, Eritrea,Libya na Misri. Maafisa wa Libya walisema zaidi ya wahamiaji 130 waliokolewa.

Filippo Grandi, kamishna mkuu wa wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR

Kamishna mkuu wa wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR, Filippo Grandi alisema mwishoni mwa wiki ajali zinazohusu boti kuzama limekuwa janga baya lililotokea mwaka huu kwenye bahari ya Mediterranean.