Miili 200 yapatikana chini ya jengo lililoharibiwa na mabomu Mariupol

maiti wakizikwa katika makaburi ya pamoja Mariupol, Ukraine

Miili ya watu 200 imepatikana chini ya mabaki ya jengo lililoharibiwa kutokana na mashambulizi ya wanajeshi wa Russia nchini Ukraine.

Wafanyakazi waliokuwa wakichimba chini ya mabaki ya jengo hilo lililokuwa linakaliwa na watu mjini Mariupol, walipopata miili hiyi ambayo tayari ilikuwa imeanza kuoza n akutoa harufu mbaya.

Mji wa Mariupol ulikumbwa na mapigano makali yaliyomalizika wiki iliyopita baada ya wapiganaji 2,500 waliokuwa katika kiwanda cha kutengeneza chuma cha Azov, kuondoka.

Wanajeshi wa Russia wamedhibithi sehemu zingine za mji huo.

Idadi kubwa ya watu 100,000 waliosalia mjini humo hawana chakula, maji, wala umeme.

Maafisa wa Ukraine wanasema kwamba karibu watu 21,000 wameuawa, na wanashutumu Russia kwa kujaribu kuficha ukweli kwa kutumia mitambo ya kuchoma maiti.

Kuna ripoti kwamba idadi kubwa ya watu waliouawa walizikwa katika makaburi ya pamoja.