Muwekaji sawa masuala ya kisiasa wa Donald Trump, Michael Cohen, alitoa ushahidi Jumatatu kwamba mgombea urais wa Marekani alimuamuru afanye malipo ya siri la dola 130,000 ili kumnyamazisha nyota wa filamu za ngono Stormy Daniels mwaka 2016 siku chache kabla ya uchaguzi.
Cohen alisema malipo yalikuwa kumzuia Daniels kutozungumza kuhusu mahusiano yake na Trump, na halafu Trump alimlipa Cohen akijidai kuwa ujira wake kwa shughuli zake za kisheria. Cohen alitumia saa kadhaa kizambani kutoa ushahidi kwenye mahakama ya New York dhidi ya mkuu wake wa zamani katika kesi ya kwanza ya uhalifu kuwahi kufanyika kwa Rais wa Marekani.
Trump anashutumiwa kwa makosa 34 kwa kugushi rekodi zake za biashara katika taasisi yake ya Trump inayohusika na biashara ya majumba ili kuonyesha kama malipo kwa Cohen ya mwaka 2017 yalikuwa kwa kazi yake ya kisheria badala ya malipo kwa kumnyamazisha Daniels.
Cohen alimkariri Trump akisema “ Hakuna sababu ya kuyaweka haya mambo hadharani fanya unavyoweza,” kwahiyo alinieleza mimi ‘nifanye ninachoweza.’ Cohen alisema kwamba baada yay eye na afisa mkuu wa masuala ya fedha wa taasisi ya Trump, Allen Weisselberg walibuni mpango wa jinsi ya kumlipa Daniels na kwamba Cohen baadaye atalipwa, walimueleza Trump na yeye alijibu “Vizuri.’