Wanafunzi wanaolalamikia ukosefu wa ajira wamekuwa wakilalamikia sheria inayohifadhi asilimia 30 ya ajira za serikali kwa wanafamilia wa wanajeshi waliopigana vita vya uhuru wa Bangladesh vya 1971.
Sheria hiyo ilisimamishwa kwa muda 2018, baada ya maandamano ya wanafunzi, lakini Juni mwaka huu mahakama iliirejesha, na kupelekea maandamano ya kitaifa. Maandamano hayo yamekuwa changamoto kubwa kwa serikali ya Bangladesh tangu waziri mkuu Sheikh Hasin, kushinda muhula wa nne mfululizo Januari mwaka huu, zoezi ambalo lilisusiwa na vyama vikuu vya upinzani.
Vyuo vikuu vimefungwa kote nchini kufuatia maandamano hayo, huku huduma za internet zikikatwa, pamoja na watu kuamurishwa kubaki nyumbani. Kutokana na kutokuwa na mawasiliano, haijabainika iwapo wanafunzi waliokuwa wakigoma wameridhishwa na uamuzi huo wa mahakama. Kufikia sasa serikali haijatoa idadi ya watu waliokufa kutokana na maandamano hayo yalioanza mwanazoni mwa wiki, lakini magazeti manne nchini yameripoti idadi ya zaidi ya watu 100.