Serikali ilijaribu kuwahimiza marubani wa moja wapi ya shirika kuu la ndege barani Afrika kutofanya mgomo wao, lakini inaonekana juhudi hazikufanikiwa.
Abiria wengi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, wamewaambia waandishi habari kwamba hawakua na habari kuhusu mgomo huo hadi walipofika kuchukua ndege.
Lawrence Ndivo aliyekua anasafiri kwa ajili ya biashara, anasema aliarifiwa uwanjani kwamba safari imefutwa.
"Waliniambia nisiwe na wasi wasi niwasili kwa muda ulopangwa. Nilijisajilisha kupitia mtandao lakini nilipowasili hapa ndipo wameniarifu juu ya mgomo huu." alisema Ndivo
Shirika la marubani wa Kenya linasema wakurugenzi wa Kenya Airways walikata kusikiliza madai yao na mapendekezo ya namna kutanzua malalamiko yao kuhuiana na mishahara na malipo ya kustahafu.
Waziri wa usafiri Kipchumba Murkomen amewalaumu marubani kwa kutupa mazuri na mabaya kwa kutotanzua mabaya.
Akizungumza na waandishi habariJumamosi waziri amesema mgomo huo umesababisha abiria elfu 10 kukwama hadi hivi sasa. Aliongeza kusema ikiwa mgomo utaendelea basi utatahiri sektambali mbali za uchumi hasa utali .