Shirika la afya duniani limeonya kwamba mamilioni ya watu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wanakabiliwa na mgogoro mkubwa wa adya na kibinadamu kutokana nan a kuongezeka mapigano na machafuko mashariki mwa nchi hiyo.
WHO limesema kwamba kuongezeka kwa vita vya makundi yenye silaha, hasa M23 linaloungwa mkono na serikali ya Rwanda japo Rwanda kudai madai hayo, kunapelekea idadi kubwa ya watu kukoseshwa makwao, kusambaa kwa magonjwa, dhuluma za kijinsia na msongo wa mawazo.
Afisa wa maswala ya dharura wa WHO Dr. Adelheid Marschang, ameambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba DRC sasa ina idadi kubwa ya watu kote duniani wanaohitaji msaada wa kibinadamu.
Jumla wa watu milioni 25.4 wameathirika.
Marschang amesema kwamba DRC inasalia kuwa nchi ambayo haipokei ufadhili wa kutosha licha ya mgogoro mkubwa, hatua inayoathiri uwezo wa watu kupokea msaada.