“Jeshi la polisi la taifa huko Rouen lilimzuia mapema Ijumaa asubuhi mtu aliyejihami kwa silaha ambaye alionekana wazi anataka kuwasha moto katika sinagogi mjini humo,” Waziri wa Mambo ya Ndani Gerald Darmanin aliandika katika mtandao wa X, uliokuwa ukijulikana kama Twitter.
Polisi waliitikia wito saa 12:45 za asubuhi (0445GMT) kuhusu taarifa ya “ moto karibu na sinagogi,” chanzo cha polisi kilieleza.
Chanzo ambacho kiko karibu na tukio hilo kiliiambia AFP kuwa mtu huyo “ alikuwa na kisu na chuma, alijaribu kuwafikia polisi, ambao walimpiga risasi. Mtu huyo amefariki.”
“Siyo tu jamii ya Wahayudi iliyoathirika. Ni mji wote wa Rouen umepigwa na butwaa na kuumia,” Meya wa Rouen Nicolas Mayer-Rossignol aliandika katika mtandao wa X.
Aliweka wazi kuwa hakuna muathirika mwingine zaidi ya mshambuliaji.