Majimbo 33 ya Marekani yanashitaki kampuni inayomiliki mitandao ya kijamii ya Meta, ikishutumu kuathiri afya ya akili ya vijana kupitia uraibu wa namna mitandao hiyo ilivyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa Jumanne katika mahakama ya serikali kuu mjini Oakland, California, ikishutumu Meta kwa kuweka vitu vinavyo sababisha uraibu katika mitandao yake ya kijamii ya Instagram na Facebook.
Vilevile inashutumi kampuni hiyo ya mtandao kuchukuwa taarifa za vijana wadogo walio chini ya miaka 13 bila wazazi wao kuruhusu ikivunja sheria ya serikali kuu.
Mlalamikaji amesema utafiti unaonyesha vijana wadogo wanaotumia mitandao ya kijamii ya Meta wanakutwa na matatizo yanayo husiana na msongo wa mawazo, wasiwasi, na kuingiliwa kimasomo na maisha ya kila siku pamoja na mambo mengine mabaya.
Kampuni ya Meta, imejibu mashitaka hayo kwa kusema imeanzisha vipengele zaidi ya 30 kwa ajili ya kuwalinda vijana hao na familia zao.