Operesheni ni kama njia ya kushinikiza Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Hamas kwenye Ukanda wa Gaza. Kuzama kwa meli hiyo kwa jina Rubymar iliyokuwa na bendera ya Belize, kumetokea wakati meli za mizigo kutoka Asia na Ulaya zikiendelea kuathiriwa na mashambulizi ya wa-Houthi, baadhi zikilazimika kutafuta njia mbadala.
Kuzama kwa meli hiyo huenda kukaongeza idadi ya meli zinazotafuta njia mbadala na kupelekea kuongezwa kwa bima, kuongezeka kwa bei za bidhaa, pamoja na kuathiriwa kwa shuguli za uchukuzi wa meli wa kieneo kwa ujumla. Serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa, pamoja na afisa wa kundi la kijeshi lililopo huko wamedhibitisha kuwa meli hiyo ilizama.
Afisa huyo alizungumza bila kujitambulisha kwa kuwa hakuwa na idhini yoyote ya kuongea na vyombo vya habari. Meneja wa meli hiyo mwenye makao yake Beirut hakupatikana ili kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo. Serikali ya Yemen iliopo uhamishoni , na inayoungwa mkono na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia tangu 2015, imesema kwamba Rubymar, ilizama Ijumaa jioni kufutia mawimbi makubwa kweye bahari ya Shamu.