Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran limeikamata meli ya mafuta yenye bendera ya Togo, inayosimamiwa na Falme za Umoja wa Kiarabu (UAE) iliyokuwa na tani 1,500 za mafuta, IRGC na kampuni ya usalama ya Uingereza ya Ambrey zimesema Jumatatu.
Meli hiyo ilikuwa imepakia mafuta ya gesi baharini katika pwani ya Iraq na ilikuwa ikielekea Sharjah, UAE ilipozuiliwa Jumapili, kilomita 112 kusini magharibi mwa bandari ya Bushehr ya Iran, Ambrey imesema.
Jeshi la wanamaji la walinzi wa Mapinduzi ya Iran limethibitisha kuikamata meli hiyo katika taarifa iliyonukuliwa na shirika la habari la serikali ya Iran, ikisema “meli hiyo ya mafuta ilikuwa ikitumiwa kusafirisha mafuta na ilikamatwa katika eneo la pwani ya Bushehr kwa amri ya mahakama.”
Meli hiyo, pamoja na wafanyakazi wake 12 wa raia wa India na Sri Lanka, imehamishiwa kwenye eneo la Bushehr na iko chini ya ulinzi shirika hilo lilinukuu taarifa hiyo.