Mamlaka ya mfereji wa Suez imesema Jumapili kuwa imefikia makubaliono ya ridhaa na wamiliki wa meli kubwa iliyokwama kwenye mfereji huo kwa karibu wiki moja mapema mwaka huu na kusababisha hasara kubwa kutoka na kuathiri safari za meli ziingine.
Hata hivyo mamlaka hiyo haijafichua ni kiasi gani cha fedha kitakacho tolewa na kampuni ya Japan ya Shoei Kisen Kaisha, inayomiliki meli hiyo kwa jina Ever Given.
Taarifa zimeongeza kusema kuwa mkataba huo utatiwa saini hapo Jumatano kwenye mji wa Ismailia kunako patikana mfereji wa Suez ambapo pia meli hiyo iliyoshikiliwa tangu wakati huo itaachiliwa. Meli hiyo ilikwama kwenye mfereji huo hapo Machi 23 kabla ya kuondolewa siku sita baadaye kwa kutumia boti kadhaa kuivuta.
Tangu wakati huo imeshikiliwa pamoja na wengi wa wafanyakazi wake wakati mashauriano kuhusu ridhaa yakiendelea